Shughuli za KDI zaanza tena baada ya Athari za UVIKO-19
Baada ya takriban miaka minne ya athari za maradhi ya UVIKO-19, asasi ya kijamii ya Kilimanjaro Dialogue (KDI) nchini Tanzania imeanzisha tena shughuli zake jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha wadau wa habari ambao katika mazungumzo walikazia umuhimu wa tasnia ya habari katika Afrika kwenda kidigitali zaidi ili kukidhi mahitaji sa kisasa ya kupashana habari…
